Nimekombolewa na Yesu
1.Nimekombolewa na Yesu Aliyenirehemia; Kwa bei ya mauti yake Nimekuwa mtoto wake. Kombolewa! Nakombolewa na damu; Kombolewa! Mimi mwana wake kweli. 2.Kukombolewa nafurahi, Kupita lugha kutamka; Kulionyesha pendo lake, Nimekuwa mtoto wake. 3.Nitamwona uzuri wake, Mfalme wangu wa ajabu; Na sasa najifurahisha, Katika neema yake. 4.Najua taji imewekwa Mbinguni tayari kwangu; Muda kitambo atakuja, Ili alipo, niwepo.