Nimekombolewa na Yesu

1.Nimekombolewa na Yesu
Aliyenirehemia;
Kwa bei ya mauti yake
Nimekuwa mtoto wake.
Kombolewa!
Nakombolewa na damu;
Kombolewa!
Mimi mwana wake kweli.
2.Kukombolewa nafurahi,
Kupita lugha kutamka;
Kulionyesha pendo lake,
Nimekuwa mtoto wake.
3.Nitamwona uzuri wake,
Mfalme wangu wa ajabu;
Na sasa najifurahisha,
Katika neema yake.
4.Najua taji imewekwa
Mbinguni tayari kwangu;
Muda kitambo atakuja,
Ili alipo, niwepo.

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Tenzi za Rohoni: Bwana u sehemu yangu