Tenzi za Rohoni: Bwana u sehemu yangu

Bwana U sehemu yangu 
Rafiki yangu, wewe 
Katika safari yangu 
Tatembea na wewe .
Pamoja na Wewe 
Pamoja na Wewe  
Katika safari yangu
Tatembea na Wewe.

Mali hapa sikutaka 

Ili niheshimiwe
Na yanikute mashaka
Sawasawa na Wewe 
Pamoja na Wewe  
Pamoja na Wewe  
Heri nikute mashaka
Sawasawa na Wewe.

Niongoze safarini
Mbele unichukue
Mlangoni mwa mbinguni
Niingie na Wewe  
Pamoja na Wewe (2x)
Mlangoni mwa mbinguni 
Niingie na Wewe
.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Nimekombolewa na Yesu